JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI - Dar East Project

Post Top Ad

JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI

JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI

Share This
Na Richard Mwaikenda, Msoga.
.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)
Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.
Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa wakati wa mauzo.
Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.
Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.
Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo kuweka majagi mawili badala ya debe moja.Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne. Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akifurahi kuona papai alililopelekewa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen) walipokwenda kumpa elimu kuhusu kilimo bora cha zao hilo nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange.
 Dk. Kikwete akishukuru kwa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mwanachama wa Mkikita  Mtaalamu wa Kilimo cha Papai kutoka Kampuni ya Awino Farm, Ezra Machogu. Kulia ni Adam Ngamange. Meneja  Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa kilimo cha Papai,  Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi
Read more


Habari Zinazoendana
8 months ago
Mwananchi

13 May
KILIMO BIASHARA: Tajirika na kilimo cha papai
Karibu katika safu mpya ijulikanayo kwa jina la ‘Kilimo biashara’. Hii itakuwa safu maalumu kwa ajili ya kuonyesha namna mkulima anavyoweza kulima kwa mtazamo wa kibishara badala ya kilimo cha mazoea au cha kuhemea tumbo.


4 months ago
Michuzi
WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) Mkakati wa Dkt. Kissui Stephen Kissui akielezea malengo ya ziara YA Wakulima wanachama wa mtandao huo walipowasili katika eneo la shamba hilo lililopo Ruaha- Kware, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, patakapolimwa zao la kibiashara la Papai. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa mtandao huo, Adam Ngamange, Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kilimo na Mifugo wa Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, John Mchopa, na...


2 years ago
Michuzi
BENKI YA KILIMO YAASWA KUTOA ELIMU KUHUSU KILIMO BORA.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,  Bw. Lephy Gembe (Katikati) akizungumza na maafisa wa kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Wapili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (Kulia) na Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw. George Nyamrunda (Kushoto). Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Robert...


8 months ago
Mwananchi

27 May
KILIMO BIASHARA: Umefikiria kulima papai?
Kilimo  kimeendelea kuwa na tija na kuleta sura ya kijasiriamali. Vijana wengi sasa wamejikita katika kilimo cha kisasa.


4 years ago
Tanzania Daima

29 Apr
Kilimo bora cha chikichi ni utajiri kwa mkulima

CHIKICHI hutoa mafuta ya mawese na hulimwa zaidi katika Mkoa wa Kigoma. Zao hili lina soko kubwa duniani, hivyo kama litaendelezwa vizuri linaweza kuwasaidia wakulima wadogo kuondoka katika wimbi la...


4 months ago
BBCSwahili
Kilimo bora cha kisasa kinaweje kuwafaidi wakulima Tanzania?
Sekta ya kilimo imekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania ambapo mwaka uliopita ilichangia asilimia 29.1 ya pato la jumla la taifa.


2 months ago
Michuzi
SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU UFANYAJI KILIMO BORA CHA MBOGAMBOGA
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO, DODOMA
Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuweza kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga katika maeneo sahihi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Aweso wakati akijibu swali la Mhe. Zainabu Amiri kuhusu Mpango wa Serikali wa kuwapatia maji safi na salama wakulima hao wa mbogamboga.
Mhe. Aweso amesema kuwa Wizara ya Maji kwa kuzingatia umuhimu wa afya za wananchi inaendelea kutoa miongozo na ushauri kuhusu...


8 months ago
Michuzi
DED MEATU: MBEGU BORA, KILIMO CHA MKATABA MKOMBOZI KWA WAKULIMA WA PAMBA

Na Stella Kalinga, Simiyu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza amesema Matumizi ya Mbegu bora na Kilimo cha Mkataba ni suluhu ya wakulima wa pamba inayoweza kuwasaidia kuongeza uzalishaji.

Manoza ameyasema wakati akitoa taarifa ya Wilaya ya Meatu kuhusu kilimo cha Pamba kwa Wakuu wa Mikoa nane ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba waliotembelea eneo hilo kutoka Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma, Singida na Tabora katika ziara yao kuona mashamba...


3 years ago
Michuzi
NAIBU WAZIRI WA KILIMO AZINDUA KIWANDA KIPYA CHA KUZALISHA MBEGU BORA ZA MAHINDI JIJINI ARUSHA
Kampuni ya mbegu ya Seedco imezindua kiwanda kipya cha kuzalisha mbegu bora za mahindi na nafaka nyingine kitakachowasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija na kupata mazao mengi.
Uzinduzi huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi ambaye alifungua rasmi kiwanda hicho ,Amesema kuwa tasnia ya mbegu ni tasnia muhimu katika ukuaji wa sekta ya kilimo hiyo amewataka wazalishaji mbegu kuongeza tija ili kukuza kilimo.
Ameeleza kuwa kampuni hiyo imetimiza matakwa ya serikali...


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here