UFUGAJI BORA SAMAKI AINA YA SATO - Dar East Project

Post Top Ad

UFUGAJI BORA SAMAKI AINA YA SATO

UFUGAJI BORA SAMAKI AINA YA SATO

Share This

UFUGAJI BORA SAMAKI AINA YA SATO


1.0 UFUGAJI WA SAMAKI
Ø  Ni kitendo cha kuzalisha samaki katika mabwawa, matenki au  Mifereji kwa lengo la chakula au kujipatia kipato

1.1 UMUHIMU WA UFUGAJI WA SAMAKI
Ufugaji wa samaki unazo faida mbalimbali ambazo ni:-
Ø  Kujipatia chakula bora na cha kutosha kwa ajiri ya familia na jamii.
Ø  Njia bora ya kujiajiri na kujiongezea kipato kutokana na mauzo ya samaki.
Ø  Hutoa fursa ya matumizi ya ardhi isiyofaa kwa ajili ya kilimo.
Ø  Ufugaji wa samaki hutoa nafasi ya kilimo mseto cha samaki na mazao/mifugo kwa wakati mmoja katika eneo moja, hivyo kutoa mavuno mengi.

1.2.0  MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI;
1.2.1Mtaji
Ø  Mkulima anashauriwa kuhakikisha kuwa ana mtaji kabla hajaamua kufanya ufugaji wa samaki, kiwango cha mtaji kitategemea ukubwa wa mradi husika.
1.2.2        Soko
Ø  Ni vyema kujua upatikanaji wa soko pamoja na washindani wako kabla ya kuanzisha shughuli hii, japo kwa nchi yetu soko la samaki ni kubwa sana, hii inatokana na uhitaji mkubwa wa samaki katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
1.2.3        Elimu
Ø  Mkulima anapaswa kuwa na elimu ya kutosha  kuhusu samaki na jinsi ya kufuga ili aweze kuendesha mradi kwa urahisi, hivyo mkulima anaweza kutafuta mtaalam kutoka vyuo vya serikali au binafsi.
1.2.4        Upatikanaji wa mbegu(vifaranga) pamoja na chakula.
Ø  Mkulima anashauriwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbegu bora na chakula cha kutosha kwa ajili ya kulisha samaki.
1.2.5        Eneo la kufugia samaki
Ø  Ni vyema pia kutafuta eneo zuri kwa ajili ya kuchimba bwawa la kufugia samaki kwa kuzingatia upatikanaji wa maji kwa wakati wote wa msimu wa ufugaji, aina ya udongo, usalama na upatikanaji wa miundombinu husika (barabara, nishati ya umeme).

2.0       AINA YA SAMAKI;
2.1       Utafiti umefanyika katika nchi nyingi na kuonelea kuwa samaki aina ya perege/ngege/sato [tilapia] anafaa kufugwa katika mabwawakulinganisha na aina nyingine.       
2.2       Samaki wa aina hii wana sifa nzuri sana kwani; huishi kwenye maji yenye joto la kadri katika nchi nyingi, wanaweza kuzaana kwa wingi katika mabwawa, hula majani na chakula kingine chochote kinachopatikana kwa urahisi shambani au nyumbani, hukua kwa haraka, uvumilia sana changamoto za bwawa hii ikiwa ni  mabadiliko ya joto, hewa ya oksijeni, na pH, pia nyama ya samaki hawa ni tamu  na yenye ladha nzuri.
2.3       Kuna aina nyingi za sato(tilapia) kama vile Sato mwekundu, Sato wa Msumbiji, Sato mweupe na Sato wa Mwanza.                                                                                      
            Sato hawa hula mimea na majani, huhitaji chakula kingi na huzaana sana, wana doa moja kubwa kwenye pezi la   mgongoni. Sato hawa hula vijimea vya plankiton, hukua kwa haraka na wana mistari kwenye mikia. Aina nyingine za samaki zimechanganyikana na kuwa machotara hivyo siyo rahisi kuwatambua.
2.4       Sato wa  Mwanza ni moja kati ya aina ya tilapia inayoshairiwa kufugwa na wataalamu wengi kwa kuzingatia sifa mbalimbali tofauti na aina nyingine.

3.0    ENEO LINALOFAA KWA UFUGAJI WA SAMAKI AINA YA SATO:
3.1.1 Upatikanaji wa maji
3.1.1 Maji ni moja ya hitaji muhimu katika ufugaji wa samaki. Eneo litafaa kwa ufugaji wa samaki ni lenye maji ya kutosha kuendesha shughuli zote za ufugaji kwa kipindi husika.
3.1.2 Chanzo cha maji kwenye bwawa kinaweza kuwa; mto, mfereji wa kumwagilia, au chemi chemi. Bwawa linahitaji maji mengi na sio rahisi kujazwa na ndoo. Ili kuhakikisha kuwa bwawa linakuwa na maji ya kutosha muda wote, chanzo cha maji cha faa kuwa cha kuaminika.
3.1.3 Kama mkulima ana maji ya kujaza kwenye bwawa kwa msimu, inawezekana pia kufuga samaki. Lakini mkulima ahakikishe anapanda vifaranga vya samaki mwanzo wa msimu wa maji. Hii itatoa fursa kwa samaki kukua hadi kufikia kiwango cha kuvunwa kabla ya maji kukauka.
3.1.4 Kama wakulima wanatumia chanzo kimoja cha maji ni muhimu kuanzisha utaratibu ambao utawezesha wakulima wote kutumia maji hayo bila matatizo. Wafugaji wa samaki wanaweza kujaza mabwawa wakati wowote kutegemea ni kipindi gani maji hayatumiki sana kwa matumizi mengine.
3.1.5 Ili kuhakikisha kwamba bwawa halitumii maji mengi, ni muhimu kuimarisha kingo za bwawa kwa kushindilia vizuri udongo wakati wa ujenzi wa msingi wa bwawa. Hii ina maana kwamba udongo lazima uwe na kiwango kikubwa cha mfinyanzi. Udongo ambao unatumika kutengenezea vyungu au kufyatulia matofali ni mzuri sana kwa shughuli hii. Kama udongo hauna ufinyanzi wa kutosha bwawa litapoteza maji kwa urahisi na italazimu kuongezwa kwa maji mara kwa mara.
3.2 Aina ya udongo
3.2.1 Inashauriwa kuwa udongo wa tifutifu au mchanganyiko wa tifutifu na mfinyanzi ambao una uwezo wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu unafaa zaidi kwa ufugaji wa samaki.
3.2.2 Udongo wa kichanga sio mzuri katika kushikilia maji lakini eneo lenye udongo wa aina hii linaweza kutumika kufuga samaki ikiwa mbinu mbalimbali zitatumika.
Zingatia
·         Kwa eneo lenye kichanga lakini lina upatikanaji wa maji ya kutosha mkulima anaweza kutumia mbinu ya kujaza mchanga kwenye mifuko ya saruji iliyokwisha kutumika na kuipanga kwenye kingo za bwawa ili kuimalisha kuta za bwawa. Kwakuwa mifuko inaweza kuoza kutokana na maji, inashauriwa ibadilishwe endapo kingo za bwawa zitaanza kumomonyoka na kuongeza tope ndani ya bwawa.
·         Karatasi ngumu ya nailoni yaweza pia kutumika kuzuia kupotea kwa maji na kulinda kingo za bwawa kumomonyoka.
·         Ujenzi wa kuta za bwawa kwa mawe au bwawa zima ni njia bora zaidi japo ni gharama ukilinganisha na mbinu nyingine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here