KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI : Pilipili mbuzi ni zao ambalo linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua angalau kiasi cha masaa 6 kwa siku.
Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili, undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.
Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa pH ni chini ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefika 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna
ya kuipunguza.
Kuandaa miche.
Mbegu za pilipili huoteshwa miche kwenye kitalu kabla ya kwenda kupandikizwa shambani. Pandikiza mbegu kwenye kitalu week 7 hadi 10 kabla ya kipindi ambacho umepanga kupandikiza miche shambani. Panda mbegu tatu tatu kwenye kila kishimo na chagua mbili zilizo chipua vizuri kwa ajili ya kuhamishia shambani.
Kuhamishia miche shambani.
Hamisha miche shambani ikiwa imetengeneza majani 8, ingawa kuhamisha ikiwa na majani machache au mengi zaidi haitapelekea shida yoyote.
MUHIMU…Unashauriwa kuhamisha miche shambani kwa kuzingatia mambo yafuatayo.
Siku ya kwanza kwa lisaa limoja weka miche kivulini au mahali ambapo kuna kizuizi jua la moja kwa moja lisiifikie miche. Kadri siku zinavyo kwenda ruhusu miche kupata mwanga wa jua zaidi.
Chimba mashimo marefu kuzidi urefu wa mizizi ya miche kisha changanya vyema udongo na mbolea ya Ngo’ombe. Muda mzuri wa kuhamisha miche yako shambani ni jioni au kipindi ambacho jua limefifia kuepuka miche kukauka.
Changanya sulphur (Tembe 2) kwenye maji na kumwagilia na rudia mchanganyo huu kila baada ya week mbili. Sulphur husaidia kuuwa fungus, inauwa bacteria wasio faa, kuzuia magonjwa pia huasaidi mizizi kusambaa na kukua kwa haraka na kupata virutubisho.
Mwagilia miche maji ya kutosha baada ya kuihamishia shambani hiyo husaidia kupunguza stress za mmea unapobadilishiwa mazingira. Tumia mbolea ya Miracle Gro kila baada ya week mbili.
Mahitaji ya mmea.
Pilipili ni zao lenye kuhitaji zaidi unyevu unyevu shambani ila maji yasiwe yenye ktuama. Kipindi ambacho maua yametoka na vitunda vya pilipili vimeanza kujitokeza, udongo ukiwa mkavu sana hauna unyevu wa kutosha hupelekea maua kudondoka. Epuka umwagiliaji ulio zidi mahitaji au ulio chini ya mahitaji. Unaweza kutandaza nyasi kwaajili ya kusaidia kuhifadhi unyevu shambani. Mmea huanza kutoa maua mapema baada ya kutengeneza matawi, Maua ya mmea hua na set iliyo kamilika (jike na dume) hivyo kuwa na sifa ya kuweza kujichavusha yenyewe.
Upepo, wadudu au kwakutumia mkono husaidia kuongeza uchavushaji.
MBOLEA
Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia mbolea,wakati huu tumia Yaramila winner 5-10g kwa mche.NB:Usitupie juu..hakikisha mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na mmea,weka 4-6 cm kutoka kwenye mmea.
Na kila baada ya siku 21 weka mbolea aina ya Yaramila winner au NPK Isipokuwa wakati maua yameanza weka Yaramila nitrabo au CAN 10g /plant,na baada ya hapo utaendelea na Y-winner mpaka mwisho wa mavuno.
KUPALILIA
Pilipili zi zao ambalo halina mizizi merefu sana, hivyo basi mkulima anapaswa kuzingatia hilo na kuongeza umakini wakati wa kupalilia kuepuka kukata mizizi.
MAGONJWA
Fusarium wilt (Mnyauko)
Njinsi ya kuepuka. .Tandika shamba lako na majani makavu ili kupunguza joto.
Ng’oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki.
Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba na chini ya miguu uingiapo shambani.
Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya kutosha.
Pulizia dawa ya fangas kama vile ortiva.
2) Southern blight ( Sclerotium wilt)
Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea muda mfupi kipindi cha joto kali.
Kuepuka/Kuzuia.
Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi waende chini sana ambapo mizizi haifiki.
Mimea iliyoshambuliwa…Ing’oe yote na choma moto lakini chomea nje ya eneo la shamba.
Pulizia Ortiva.
3) Anthracnose.
Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa huweza kukaa ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama kuna sehemu zinakuwa nyeusi na panajaa majimaji …dalili hii huenea sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.
Kuepuka.
Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu..Baada ya kuvuna choma mabaki yote.
Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo zaidi ya mara mbili…badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio jamii moja na pilipili mbuzi (Do crop rotation).
Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu…kwa hiyo mkulima lazima achukue mbegu kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na mwaminifu…mbegu hazitakiwi kutengenezwa kutoka kwenye mimea iliyoathirika na ugonjwa.
4) Bacteria.
Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda….huweza kutokea na kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.
Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na pia kwenye matunda.
Kuepuka.
Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu ugonjwa.Nunua kutoka kwa wakala.
Pulizia dawa yoyote copper.
5) Virusi.
Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili mbuzi.
Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .
Kuepuka.
Nunua mbegu bora
Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na kuendelea.Wadudu wanaosababisha virus sanasana na wadudu mafuta (Aphids) kwa hiyo akikisha muda wote shambani hakuna hao wadudu kwa kupulizia Actara.
NB:Pamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila kupiga dawa ya wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna ugonjwa.
Wadudu.
Pilipili mbuzi hushambuliwa na ;
Wadudu mafuta ( Aphids)
Kuwadhibiti.
Tumia Actara 8g/20L.
Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.
Crickets
Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka walipo jificha na kukata miche michanga.
Kawadhibiti.
Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na kuwaacha katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama ni miche na iko kwenye tray…basi weka hizo tray juu ya kichanja.
Beetle.
Tuma Karate 40cm/20L.
Utitiri
Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.
Nematodes
Tumia solvigo.
Mavuno.
Pilipili huwa tayari kwa kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemea na aina ya mbegu uliyotumia. Chuma kwa uangalifu bila kung’oa mmea ili uendelee kuzalisha. Muvuno yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi 1 hadi 3.
Usalama wakati wa uvunaji.
Pilipili huwa na kemikali iitwayo capsaicinoids ambayo inaweza
kukuwasha kwenye ngozi au kwenye macho ikiwa utajigusa. Vaa gloves wakati wa kuvuna na kuwa mwangalifu usijiguse kwenye macho.
SOKO
Fursa
Pilipili ni zao ambalo halina mbadala wake au (substitute) hivyo kufanya mahitaji yake kuwa ni ya muda wote bila kutetereka.
Changamoto
Muda ambao wakulima wengi wanakuwa wamezizalisha zaidi huathiri sana soko la pilipili kwa maana hata bei ikishushwa sana haiwezi kushawishi watumiaji kutumia pilipili nyingi zaidi.
Kuepuka changamoto hiyo wakulima wanashauriwa kupunguza huduma shambani hadi pale soko litakapo tengemaa vizuri.
Mbinu za mafanikio kwenye kilimo hiki.
ZALISHA KWA WINGI
Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo haziepukiki yani (Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo utaweza pia uza bidhaa zako kwa bei ndogo na bado utapata faida nzuri na kujihakikishia soko la uhakika kwa bidhaa zako.
TAFUTA MASOKO YA BIDHAA KABLA YA KUANZA UZALISHAJI
Mkulima mwenye mafanikio ni lazima pia awe mfanya biashara mzuri ukiachilia mbali kuwa mzalishaji mzuri. Mkulima ni vyema kutengeneza channels mapema kupata wateja wa mazao yako. Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo itakusaidia sana kwenye kupata masoko utakwa na ushawishi zaidi kwa wateja. Tengeneza wateja na wateja watakutengenezea biashara.
Mteja anataka vitu vitatu vya msingi.
Unafuu wa bei
Ubora wa zao
Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa
Ukijihakikishia hivyo vitu vitatu hapo juu hapana shaka utakuwa umejihakikishia soko la uhakika.
USILIME KWA KUFUATA MSIMU
Unapolima kwa kufuata msimu, mtajikuta wakulima wengi mmezalisha zao fulani kwa wiiingi kwa kipindi kimoja hivyo kupelekea upatikanaji wa zao hilo kuwa mkubwa kuliko inavyo hitajika kwenye masoko, jambo hili hupelekea mazao kuuzwa kwa bei ndogo na kupelekea wakulima kukosa faida ya kutosha au hata kupata hasara muda mwingine.
Unapolima kwa kutofata msimu mkulima utaweza kuazalisha zao/mazao kipindi ambacho wengine hawazalishi hivyo mahitaji yatakuwa makubwa na upatikanaji wa zao hilo utakuwa ni mdogo hivyo mkulima ataweza kupanga bei nzuri kwa mazao yake.
USIFANYE KILIMO KWA MAZOEA
Tumia wataalamu wa kilimo
Tumia njia za kisasa za kilimo
Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka kufanya (Tumia wataalamu)
Fanya kilimo cha umwagiliaji uweze kuzalisha kipindi ambacho wengine hawawezi kuzalisha ili uuze mazao yako kwa bei nzuri zaidi,
FAIDA ZA KUTUMIA PILIPILI
Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu.
Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.
Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.
Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili.
Pilipili husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi.
Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer).
Pilipili husaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.
8. Kula pilipili husaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu
Share this:
No comments:
Post a Comment