Simba wafika fainali Kombe la SportPesa kwa kuwalaza Kakamega Homeboyz - Dar East Project

Post Top Ad

Simba wafika fainali Kombe la SportPesa kwa kuwalaza Kakamega Homeboyz

Simba wafika fainali Kombe la SportPesa kwa kuwalaza Kakamega Homeboyz

Share This
Mabingwa wa ligi ya Tanzania bara Simba wametinga fainali ya michuano ya Super Cup ya kampuni ya Sportspesa baada ya kuwacharaza Kakamega Homeboyz wa Kenya kwa mikwaju 5-4 ya penalti.

Simba walipata ushindi huo kwenye nusu fainali iliyochezewa uwanja wa Afraha, Nakuru.

Walifika nusu fainali baada ya kuwaondoa Kariobangi Sharks wa Kenya.

Klabu hiyo sasa itamsubiri mshindi wa nusu fainali kati ya mabingwa wa ligi Kenya Gor Mahia na Singida FC ya Tanzania kufahamu nani atakuwa mpinzani wao fainali.

    Simba ‘wanguruma’ Kenya, Yanga na JKU wa Zanzibar hoi

Singida FC walifika nusu fainali na kuwaondoa mahasimu wa jadi wa Gor Mahia AFC Leopards.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here