Doe na Tylor siasa zawafanya kuwa maadui - Dar East Project

Post Top Ad

Doe na Tylor siasa zawafanya kuwa maadui

Doe na Tylor siasa zawafanya kuwa maadui

Share This
NI SAMUEL DOE NA CHARES TYLOR MARAFIKI WAKUBWA WAWILI AMBAO SIASA ILIWAFANYA KUWA MAADUI WAKUBWA LIBERIA.


NA:Comred Mbwana Allyamtu.

Mpaka nafikilia kuandika hii makala ni baada ya kutafakala karibu kwa saa kama 2 hivi juu ya hili swali Kwanini marafiki wengi wa siasa mwisho wake hugeuka kuwa maadui sana tena hata kufikia hatu ya kuweza kumdhuru mwenzie?

Swali langu hili lilienda mbali hata kuwaza kuwa je urafiki wa Jakaya Kikwete na Edward Lowassa ambao hata wao walikili kuwa sio wa barabarani ambao baadae uligeuka kuwa fahali wawili wenye kunyukana. Pia sikuishia hapo ni kule Africa ya kusini kati ya Jacob Zuma na Thambo Mbeki waliokuwa marafiki na baadae kuwa maaadui hata kufikia Mbeki kutaka kummaliza Zuma kisiasa kwenye sakata la Ngono. 

Wote tunajua juu ya urafiki wa Nyerere na Kambona ulipoishia na nyerere na Mzee Jumbe ulipohitimishwa kwa Jumbe kuwekwa kizuizini huko mji mwema mpaka kifo chake. Wote tunakumbuka uswahiba wa Thomas sankara na Brasius Brasana Compoule ulipo ishi kwa Compoule kumdhururu Sankala kwa kumuua. Pia historia hutukumbusha yale ya Laulent Kabila na Andre Kisasi Ngando na AFDRL kule kongo-DRC wakati wa kumuondoa Mubutu madalakani. Listi kama hii ni ndefu sana hata siwezi kuimaliza kuitaja......

Hali hii huendelea mpaka kule ughaibuni alkadhalika urafiki katika siasa mwisho ugeuka kuwa "uadui". Hatujui kule Kenya kati ya Ruto na Uhuru kama watafika salama na Jubilei yao.
Nimeamua kuandika makala hii kusadifu hali hii ya urafiki wa siasa namna unavyoweza kuwa uadui na history imekuwa ikituonesha hivyo. Ni vyema sasa tukaipitia hii historia ya Doe na Tylor tukajifumza kitu.....

CHARLES TAYLOR NI NANI?
Charles McArthur Ghankay Taylor, amezaliwa Januari 28, mwaka 1948. Taylor ni Rais wa 22 wa Liberia, akiwa ametumikia nchi hiyo kuanzia Agosti 2 mwaka 1997 hadi alipojiuzulu Agosti 11, mwaka 2003. Taylor aliingia AGOSTI 2 (1997) akang’oka AGOSTI 11 (2003). Taylor alizaliwa Arthington, Jimbo la Montserrado nchini Liberia, ni msomi aliyepata shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Bentley Marekani na alipata kufanya kazi katika Serikali ya Samuel Doe. Baada ya kung’olewa katika serikali hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu alikwenda Libya ambako alipata mafunzo ya kuwa mpiganaji wa msituni.

Alirudi Liberia mwaka 1989 akiongoza kundi la upinzani lililoitwa National Patriotic Front of Liberia, lililokuwa na lengo la kuung’oa utawala Samuel Doe, Taylor akawa mwanzilishi wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya kwanza nchini Liberia, kati ya mwaka 1989 hadi 1996. Baada ya mauaji ya Samuel Doe, Taylor akawa na nguvu katika eneo kubwa la Liberia, akitambulika kuwa miongoni mwa wababe wa kivita vinara Afrika. 

Kutokana na kuwapo kwa mpango wa amani uliolenga kukomesha mapigano Liberia, Taylor akiwa na umaarufu wa kutosha hatimaye akachaguliwa kuwa Rais wa Liberia, mwaka 1997. Akiwa ofisini, Taylor alikumbwa na kashfa mbalimbali za uhalifu wa kivita na hata ukatili dhidi ya binadamu, akitajwa kuhusika katika uchochezi wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone, mwaka 1991 hadi 2002.

Ndani ya nchi yake, upinzani dhidi yake ulishamiri na kuzusha vita nyingine ya wenyewe kwa wenyewe ya pili kati ya mwaka 1999 hadi 2003. Lakini katika mwaka huo wa 2003, Taylor alikuwa amepoteza sehemu kubwa ya nguvu zake pembezoni mwa nchi na mwaka huo huo alijiuzulu baada ya kuwapo kwa shinikizo kubwa la kimataifa na akatoroka kwenda uhamishoni nchini Nigeria.

Alikutwa na hatia katika Mahakama ya Kimataifa Aprili mwaka 2012, kwa makosa 11, yakiwamo ugaidi, mauaji na ubakaji. Mei mwaka 2012, Taylor alihukumiwa kifungo cha miaka 50 jela. Kama ilivyo kwa Compaore aliyesaidia mapinduzi yaliyomweka madarakani Sankara, Taylor naye alisaidia mapinduzi ya kijeshi ya Aprili 12, mwaka 1980 yaliyokuwa yakiongozwa na Samuel Doe, ambayo hatimaye yalisababisha mauaji ya Rais wa wakati huo wa Liberia, William R. Tolbert na Doe akaingia Ikulu.

Kwa kumbukumbu tu ni kwamba, Rais Tolbert aliwahi kutoa mhadhara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wasomi wa wakati ule wa ujana wao, akina Profesa Issa Shivji na wengine wengi wanafahamu hili, kimsingi Tolbert alikuwa rafiki wa Tanzania pamoja na Rais Julius Nyerere. Baada ya Doe kuingia madarakani, Taylor aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Jumla wa Huduma (GSA), akiwa na mamlaka ya kufanya ununuzi unaohitajika kwa Serikali ya Liberia. Alifukuzwa kwa ubadhirifu Mei mwaka 1983 akitajwa kufuja dola za Marekani takriban 1,000,000 na kuzituma katika akaunti yake katika moja ya benki zilizoko Marekani.

Baada ya ubadhirifu, Taylor alitorokea Marekani lakini alikamatwa Mei 21 mwaka 1984 na kurudishwa Liberia kujibu mashtaka ya ubadhirifu wa fedha za serikali dola za Marekani milioni moja, alipokuwa bosi wa GSA. Septemba 15 mwaka 1985, Taylor na wafungwa wenzake wengine wanne walitoroka jela. Desemba 1989, Gaddafi, mbali na kumwezesha Taylor kupata mafunzo kama mpiganaji wa msituni pia alisaidia upatikanaji wa fedha kupitia mfuko maalumu ulioratibiwa nchini Ivory Coast ambao fedha zake ndizo zilizompa nguvu Taylor kumng’oa Samuel Doe, na kupitia vita ya kwanza ya wenyewe kwa wenyewe Liberia.

Kati ya mambo ya kukumbukwa ni pale mara baada ya kuhimitishwa kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Liberia (ya kwanza) mwaka 1996, Taylor akiwa anagombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 1997. Alikuwa akifanya kampeni akitumia kaulimbiu mashuhuri kwamba “..amemuua mama, amemuua baba lakini nitampigia kura. Kama ambavyo Gaddafi alimsaidia Taylor kumng’oa Samue Doe kwa kuanzisha vita ya wenyewe kwa wenyewe, ndivyo hivyo pia Taylor naye akiwa Rais anadaiwa kusaidia kuanzishwa kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone, akitajwa kuwasaidia waasi wa Revolutionary United Front (RUF) kwa kuwauzia silaha.

Katika harakati zake na hasa pale alipokuwa akituhumiwa kwa kufanya mauaji, Taylor amekuwa akitamka kwamba; “...hata Yesu alituhumiwa kwa mauaji nyakati zake.”
Kwa shinikizo kama ilivyo kwa Compaore, Taylor naye alijitokeza kwenye televisheni Agosti 10, akitangaza kwamba ataachia madaraka siku inayofuata kwa Makamu wa Rais Blah.

SAMUEL DOE NI NANI?
Samuel Kanyon Doe alizaliwa May 6, 1951 jijini Tuzon, nchini Liberia Alfajiri ya Aprili 12, 1980, kikundi kidogo cha wanajeshi 17 kilijipenyeza ndani ya makazi ya Rais jijini Monrovia. Ikulu walimkuta Rais William Tolbert bado amelala Wakamuua Aliyeongoza kikundi hicho alikuwa askari kijana na wa cheo cha chini, Sajenti Samuel Doe Na inasemwa kuwa Doe alipoingia Ikulu na wenzake, alidhani watakwenda kumlalamikia Rais juu ya mishahara midogo ya askari wa vyeo vya chini... 

Lakini jinsi walivyoikuta Ikulu ikiwa nyepesi vile, ndivyo mipango ilipobadilika na kuamua kumuua Rais mwenyewe na kuchukua madaraka. Samuel Doe alikuwa askari ambaye hata madarasa manne ya shule ya msingi hakuyamaliza... Alitoka kabila dogo la waishio misituni, kabila la Krahn... Ni watu wa kabila kama lake, masikini na ambao ndio waliotoka vijijini na kukimbilia jijini Monrovia kutafuta vibarua na pesa... Kwa wenye bahati, kama Samuel Doe, walionekana mitaani na kuitwa kujiunga na Jeshi.

Na kama ilivyokuwa kwa Idi Amin, Urais ulimdondokea tu Samuel Doe, kama vile mtu aliyeshinda bahati nasibu Ujio wa Samuel Doe uliwafaya WaLiberia waamini kuwepo kwa mabadiliko Kuondokana na utawala wa kifisadi na kirasimu wa William Tolbert Samuel Doe akajitangaza kuwa Rais, April 12, 1980... 

Haraka sana akawatwanga risasi mawaziri wote wa Tollbert... Ni kwenye pwani ya bahari huku wananchi wakitazama kama mechi ya mpira Sajenti Samuel Doe akatawala kwa kipindi cha miaka kumi Nchi ikawa kama imesimama. Watu wa kabila la Samuel Doe waliogopewa na makabila mengine Waliweza kufanya lolote lile na hakuna aliyewagusa… Waliua na waliwatisha wengine. 

Wengi wasio wa kabila la Rais Doe, waliishi kwa hofu kubwa Na kile ambacho kila mtu asiye wa kabila la Doe, alikuwa anakisubiri, ni kushuhudia mwisho wa Sajenti Samuel Doe Na hapa akatokea Charles Taylor… Huyu alikuwa rafiki wa zamani wa Sajenti Samuel Doe. Lakini, urafiki wao ulikufa pale Samuel Doe alipodai kuwa Charles Taylor alimtapeli dola milioni moja… 

Kisha Taylor akatorokea Marekan Huko akaanza kufanya biashara kwa mtaji wa fedha alizomtapeli Sajenti Samuel Doe Charles Taylor naye akaishia gerezani nchini Marekani kwa mashtaka ya utapeli Lakini akatoroka jela na kukimbilia Ivory Coast... Na akiwa Ivory Coast, Charles Taylor akaanza kujipanga kwenda kuuangusha utawala wa Sajenti Samuel Doe Charles Taylor akiwa Ivory Coast, alikiandaa kikosi cha wapiganaji 60 Kikosi kilikuwa tayari kwa kuingia Monrovia kumwondoa Samuel Doe madarakani.

Ilikuwa ni mwaka 1989 Wakati huo, wajuzi wa masuala ya kijeshi waliamini kabisa, kuwa Sajenti Samuel Doe angeweza, kirahisi kabisa, kumteketeza kijeshi Charles Taylor na kikosi chake cha watu 60 Sajenti Samuel Doe angeweza kufanya hivyo hata kabla Charles Taylor hajavikaribia viunga vya Monrovia Badala yake, ‘’Master Sergeant’’ Samuel Doe, aliwatuma mstari wa mbele, wanajeshi kutoka kabila lake la Krahn.

Niwanajeshi wa kuokoteza ambao wengine hawakuwa hata na viatu… Wanajeshi wale wa Samuel Doe, njiani wakitokea mji mkuu Monrovia wakielekea uwanja wa mapambano, wakaanza kufanya wizi wa ngawira, kuiba mali za watu Habari za askari ‘’vibaka’’ wa Samuel Doe zikasambaa haraka kwenye vijiji vya msituni Huko watu wakajitolea kujiunga na vikosi vya Charles Taylor kukabiliana na askari wa Samuel Doe Jeshi la Taylor likakua kwa haraka… Baada ya miezi sita tu, likaingia kwenye viunga vya mji mkuu wa Liberia, Monrovia, June 1990.

Ndipo hapo kwenye kambi ya Charles Taylor ugomvi ukazuka Nani atakuwa Rais???..Nani atakuwa na mamlaka ya hazina kuu???... Ni ugomvi uliowatenganisha Charles Taylor na Prince Johnson aliyeamua kuachana na Taylor na yeye kuanzisha kikosi chake. Wote wawili walikuwa na tamaa ya Ikulu. Vita sasa ikawa ya vikosi vitatu kugombania kuingia Ikulu ya Monrovia: 

Kikosi cha Sajenti Samuel Doe kinachojihami, kikosi cha Charles Taylor na kikosi cha Prince Johnson.Wote wakaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe kugombania Ikulu ya Monrovia.Mitaa ya Monrovia wakaonekana askari wa makundi tofauti wakipigana. Hata watoto waliingizwa kwenye vita vile vya kiwendawazimu Hatimaye, mwishoni mwa mwezi August 1990, vikosi kutoka nje viliingilia mgogoro ule... 

Ni vikosi vya Nigeria chini ya mwavuli wa ECOMOG, ni umoja wa mataifa ya Afrika Magharibi… Ecomog walikuwa na jeshi lilioongozwa na kamanda kutoka Nigeria... Jeshi hilo lilifika Monrovia na meli kubwa ya kijeshi.

Jumapili Septemba 9, 1990, Rais Samuel Doe aliposikia habari za ujio wa ECOMOG, akafanya kosa kubwa la kuamua kutoka Ikulu na kwenda mwenyewe bandarini kuonana na kamanda wa vikosi hivyo vya majeshi ya Nigeria. Samuel Doe hakuwa na msafara mkubwa. Aliwachukua walinzi wake na kuingia kwenye Mercedes Benz kuelekea bandarini Masikini, 

Rais wa nchi akajikuta anapita kwenye mji wenye miba Akafika bandarini na hapo Prince Johnson alikuwa amewapanga askari wake kumshughulikia Samuel Doe.Zikapigwa risasi na walinzi wote wa Samuel Doe wakapoteza maisha Samuel Doe mwenyewe risasi ilimpata mguuni na hakuweza kukimbia, akakamatwa Akafungwa kitambaa usoni na akapelekwa kwenye kuteswa.

Prince Johnson akahakikisha mateso yale yanarekodiwa kwa kamera za filamu... Kwenye filamu hiyo, Prince Johnson anaonekana akipungiwa upepo na mwanadada huku akinywa bia na kumwangalia rafiki yake wa zamani, Samuel Doe akiteswa… Muda mwingi Prince Johnson alikuwa akimtaka Samuel Doe aseme zilipo fedha kwenye hazina Kuna wakati alisikika Samuel Doe akimwita rafiki yake wa zamani kwa jina alilozoea kumwita: 

"Prince, waambie walegeze kamba walizonifunga, nitasema kila kitu, walegeze hizo kamba kwanza!" Ukweli, kamba walizomfunga kwenye miguu na mikono zilikaza sana na kumletea maumivu makali… Waliendelea kumpiga huku wakimtaka ataje ilipo hazina. Walimtaka ataje akaunti yake ya benki Ndivyo ilivyokuwa barani kwetu Afrika, na labda mpaka leo
View attachment 401852 

Rais dikteta anapopinduliwa, kikubwa kinachotafutwa ni namba ya akaunti ya benki alikoficha fedha… Mara nyingi ni kwenye benki za nje… Ndio, inahusu hazina ya nchi "Mkateni sikio kama hataki kusema!" Alisikika Prince Johnson akitamka kwa hasira

Askari wale wakamtupa Samuel Doe sakafuni, wakamkata sikio moja "Mkateni sikio lingine!", alisikika tena Prince Johnson akitamka Baada ya hapo, Rais Doe aliuawa kikatili Jumapili hiyo jioni, Septemba 9, 1990 baada ya kukatwa masikio yake, sehemu zake za siri na baadhi ya vidole vya miguu na mikono na hatimae mwili wake ulitembezwa mitaa mbalimbali ya jiji la Monrovia.

Huo ndio ulikuwa mwisho wa Dikteta Samuel Kanyon Doe wa Liberia… Aliopinduliwa na kuuliwa na marafiki zake ambao ndio waliomsaidia yeye kuingia ikulu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here