Historia ya Libya - Dar East Project

Post Top Ad

Historia ya Libya

Historia ya Libya

Share This

Historia ya Libya

Historia ya Libya inahusu eneo la Afrika Kaskazini ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Libya.
Wakazi asili walikuwa Waberber. Baadaye wakaja Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki upande wa mashariki.
Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma, na Ukristo ukaenea.
Baada ya dola hilo kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi.
Katika karne ya 7 Waarabu waliingiza Uislamu na utamaduni wao.
Mwaka 1551 Waturuki walifukuza Wazungu kutoka Tripoli wakatawala hadi karne ya 20.
Nchi ilitawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941.
Waingereza waliacha nchi mwaka 1951 mikononi mwa mfalme mwenyeji.
Kisha kupindua mfalme Idris I, Muammar al-Gaddafi alitawala kidikteta tangu mwaka 1969 hadi alipopinduliwa na kuuawa mwaka 2011.
Baada ya hapo wananchi wanazidi kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here