Hii ndiyo sababu ya kifo cha Sam wa Ukweli - Dar East Project

Post Top Ad

Hii ndiyo sababu ya kifo cha Sam wa Ukweli

Hii ndiyo sababu ya kifo cha Sam wa Ukweli

Share This
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa hiyo imethibitishwa na msambazaji wa nyimbo zake ambaye pia Meneja wa ‘Team Mtaa kwa Mtaa’, Amri the Business aliyeeleza kwa masikitiko alivyopokea makubwa kuwa Sam amefariki dunia.

Nae aliyekuwa mtayarishaji wa nyimbo za Sam wa Ukweli, Producer Steve amesema Sam alizidiwa zaidi Jumamosi iliyopita na walipomuuliza alisema ni ‘UKIMWI wa kulogwa’.

Sam wa Ukweli aliwahi kutamba na ngoma kama Sina Raha, Hata Kwetu Wapo, Kisiki, Milele na nyingine nyingi kali kuanzia mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here