FURSA YA KILIMO CHA PAPAI
Papai ni MATUNDA ambayo wengi tunayafahamu. Ekari moja ya papai inachukua miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu moja na mia mbili). Kwa maana ya mita mbili kwa mbili kutoka mti hadi mti na hii ni kwa ile mbegu fupi. Ukilima kwa kufuata utaalamu ni kwamba mti mmoja wa papai unaweza kutoa matunda 86 hadi 100 kwa msimu. Kutoka kupandikiza shambani hadi kuanza kuvuna mavuno ya kwanza, papai zinachukua miezi nane hadi kumi tu. Ikiwa unamwagilia papai ni tunda lisilo na msimu, yaani unavuna mfululizo......
Nimesema mti mmoja unatoa matunda 86 hadi 100 sasa kwa ajili ya kustandadaizi tuchukulie kwamba mti umekupatia matunda 80 pekee. Tunda moja la papai, kwa pale sokoni linauzwa kuanzia 1000, hadi elfu 4,000 kutegemea na ukubwa, lakini ni nadra kupata papai chini ya shilingi 1,000 kule sokoni, si ndio jamani? Sasa wewe ukilima chukulia kwamba unauza 5,00 (mia Tano tu) kila tunda kwa bei ya kujumlishia pale pale shambani(yaani hutaki mausumbufu ya kupeleka sokoni, unawaita wajumuaji wanunulie hapo hapo shambani). Ikiwa mti mmoja unatoa papai 80 maana yake kila mti utakupatia shilingi elfu arobaini, 40,000/=. Tunakwenda sawa mpaka hapo?
Sasa chukua elfu 40 zidisha mara miti elfu moja(hapa napo nimeashumu kwamba uliingiza miti elfu 1, 000 pekee). Hii itakupa hesabu ya shilingi milioni arobaini 40,000,000/= keshi! Sawa sawa?
Turejee kwenye gharama za uwekezaji, yaani tunajiuliza ni shilingi ngapi unatakiwa kutumia ili kupata hii milioni arobaini keshi? Twende na hesabu hizo...
Kitaalamu inashauriwa kwamba miti ya mipapai inatakiwa kukaa shambani kwa miaka isiyozidi mitano na baada ya hapo ing'olewe na kubadilishwa mingine. Pia inaelezwa kwamba mavuno makubwa zaidi(maximum production) unaipata kuanzia mwaka wa pili wa mavuno. Maana yake ni kwamba shamba la papai unaweza kukodi ama kununua. Kukodi ni gharama zaidi ukilinganisha na kununua. Mathalani kukodi ekari moja katika MASHAMBA ya kumwagilia kule Ruaha Mbuyuni Iringa (ambako ndio nyumbani kwa mapapai) ni shilingi laki moja kwa mwezi hivyo kwa mwaka utalipa 1.2Milioni kukodi. Wakati kununua shamba maeneo ya mahenge huko huko Iringa haitakugharimu zaidi ya milioni 2.5 kushuka chini. Lakini pia kuna maeneo mengi Tanzania ambako papai zinastawi na unaweza kununua shamba lako ekari moja hata kwa chini ya laki tano. Kwa hiyo gharama ya shamba inategemea ni wapi unakwenda kuwekeza kilimo hili. Twende sasa gharama zingine....
Kulima shamba na kuandaa mashimo, ni mambo ambayo hayawezi kukugharimu zaidi ya laki tano, yaani namaanisha ni pungufu ya hapo. Miche ya papai unaweza kuiandaa mwenyewe kwa kiwatika kwenye Kitaru ama unaweza kuinunua kwa wawatikaji. Kama ukiamua kuiandaa mwenyewe unafanya hivi: nenda sokoni ununue papai lako la buku, buku mbili au buku nne; chagua lile zuri na tamu, kisha ukishalikata chukua zile mbegu. Mbegu zile zitie kwenye maji ya vuguvugu kisha uzipekeche kwa ajili ya kuondoa ule utando. Baada ya hapo zianike kivulini lakini pawe na hewa kwa siku tatu hadi Tano; kisha zipande kwenye viriba vipana(vile vikubwa). Katika kujaza udongo kwenye viriba, hakikisha unachagua udogo wenye rutuba na uchanganye na udongo wa mchanga kwa pale juu, yaani juu ya udongo ule wenye rutuba. Baada ya wiki mbili miche itaanza kuota na baada ya miche kuota unaweka mbolea ya kuku kwa ajili ya kubusti mimea....
Hii ni kwamba ukiandaa miche mwenyewe; miche ya ekari moja itakugharimu chini ya laki moja tu (kwa maana ya kulipia maji ya kumwagilia, viriba, na mengine). Lakini pia unaweza kununua miche ambapo bei standadi kama unanunua miche mingi ni mia tano kwa mche, miche elfu moja ni shilingi laki tano. Mengine madogo madogo kama usimamizi na ufuatiliaji wewe jumlishia tu hapo. Nini NATAKA ukione hapa? Ni kwamba unaweza kuwekeza ekari moja ya papai kwa chini ya milioni 3 na ukawa na uwezo wa kupiga milioni 40 ndani ya muda wa mwaka mmoja tu. Hapa unachokosa wewe sio hela isipokuwa ni taarifa na miongozo, uwongo kweli? Twende tu, utaelewa kwa nini tunasema unatakiwa upate milioni 890.....
Sasa tuone milioni 890 inafikiwaje. Tuseme mwaka wa kwanza umejichanga weee ukalima hiyo ekari moja na ukakamata hizo milioni 40. Mwaka unaofuatia chukua milioni 15 nenda kaongeze ekari 5(kwa maana gharama za eka moja tumeona ni kama 3M kwa hiyo eka 5 ni milioni 15). Kwenye zile 25 zinazobaki mimi nakuruhusu kwa moyo mweupe ukitaka kuzitumbua zitumbue tu(ila ukikutwa na Mh. Naibu Spika, usinitaje). Okei, kama mwaka unaofuata utalima ekari zingine 5 maana yake utakuwa na ekari 6 jumla na kwa hesabu ya milioni 40 kwa ekari maana yake utavuna milioni 240, sawa sawa? Mwaka wa tatu chukua milioni 60 nenda kalime ekari 20 ambazo kwa hesabu za milioni 40 kwa ekari maana yake utapiga milioni 800 cash jumlisha na zile za ekari sita uone kama hutapata bilioni moja na ushehe! Na hapo ndio kwanza unakuwa mwaka wa NNE, hata mitano haijaisha unakuwa umeshakamata bilioni, je ikifika mitano? Ukishamiliki shamba la MATUNDA ekari 26 wewe ni level zingine kabisa, hatuongelei tena uende kuuza sokoni Tandale hapo sasa tunaongelea habari ya wewe kupeleka MATUNDA Comoro, Ufaransa, Ujerumani, Zanzibari, Ushelisheli na kwingine kwingi ambako kuna masoko ya kumwaga na kumwagika! Mpo mpaka hapo?
Kuna watu huwa wanaleta saundi za kwamba ohooo, matunda yamekosa masoko, mara ohoo yanaoza kwa kukosa wateja! Ukimsikia mtu anasema hivyo hata kama ni kwenye TV mzomee kabisa halafu jiulize maswali haya: wanaposema MATUNDA yamekosa soko ni matunda gani? Je, hayo matunda yalipandwa kitaalamu kwa wazo la kuja kuuza kisasa ama ndio ile miti ya matunda iliyojiotea tangu enzi za mababu?
Sikilizeni niwaambie: MATUNDA yana soko kubwa na soko hilo haliwezi kupotea leo wala kesho. Kuna mbunge tunae hapa bungeni amepata kunieleza kwamba kama kuna mtu ama kikundi cha watu ambacho kinaweza kujaza matunda kiwango cha kontena la futi 40 kila wiki; basi kuna wajerumani ambao wanakuja kuyavuna hayo matunda shambani. Maana yake kwenye hii nchi kunaupungufu mkubwa sana wa watu wanaolima matunda siriazi, kwa wingi na kwa misimu yote(sio tu kutegemea mvua). Mbunge mwenzetu huyu ambae ni mtaalamu na anafanya usafirishaji MATUNDA nje ya nchi, amekuwa akinisisitiza kwamba kama kuna jambo la maana tunaweza kufanya ni wabunge kulima MATUNDA siriazi kisha tukaunganisha nguvu na kuyasafirisha nje ya nchi. Kabla hujasema matunda hayana soko, hebu lima kwanza.....
Hii sasa sikupigii hesabu ila nakuachia swali: ikiwa ukiuzia mapapai yako kwa wachuuzi wa Tandale unapata mia tano kwa kila tunda; je, unadhani ukisafirisha kwenda Comoro ama Ujerumani utapata hiyo hiyo mia tano? Bila shaka hapana hata kidogo! Ukitoa manauli, maushuru, makodi na mazagazaga mengine kibao, nina uhakika huwezi kupata chini ya elfu 2 kwa kila papai moja. Bila shaka hiyo simu yako ina kalukuleta, kwa hiyo nenda kwenye hesabu zangu hapo juu, katika kila penye mia Tano, weka elfu 2 halafu hayo mahesabu kaa nayo mwenyewe!
Nafahamu unasubiria strawberries, usiwe na hofu, ninakuja huko baadae. Sasa nieleze hali ya hewa na msimu uaofaa kulima mapapai. Kimsingi mapapai yanastawi katika hali mbalimbali za hewa, lakini matokeo makubwa ya kimavuno unayapata ikiwa utayalima maeneo yenye joto na yenye maji ya kutosha iwe ni kwa mvua ama kwa kumwagilia. Unapopanda papai unatakiwa kuchimba shimo pana na refu, futi 2*2 linafaa zaidi ambapo ndani yake unaweka samadi na udongo na pale juu unatandaza vigunzi ama majani kwa ajili ya kuhifadhi unyevu. Wakati wa kiangazi unaweza kumwagilia mara nne kwa mwezi ama mara mbili kwa mwezi na bado ukapata matokeo mazuri. Sio lazima upate maeneo yenye maji ama mito, isipokuwa unaweza kuchimba kisima kidogo tu na kikatosha kumwagilia ekari nzima. Nawafahamu vijana fulani wanaoweza kusafiri mahali poppte nchini, ambao wanauwezo wa kuchimba kisima na kikatoa maji kwa chini hata ya milioni moja. Msimu mzuri wa kupanda papai ni katika wakati huu wa mvua ambapo inarahisisha miche kushika haraka, ingawa ukiwa na maji ya uhakika unaweza kupanda muda wowote.....
Changamoto zinazokabili kilimo hiki. Kwanza kabisa kuna magonjwa. Kuna ugonjwa unaitwa wa ukungu, huwa unashambulia miche ikingali midogo. Hata hivyo kuna dawa zake na unatakiwa kupiga dawa wiki ya tatu hadi NNE. Ukichelewa unadumaza miche na hata kama utaenda kununua kwa wanaowatika hakikisha kwamba unafuatilia ikiwa walipiga dawa hii. Pia wakati wa kubeba MATUNDA, yaani ule muda wa maua kuna dawa ya kuzuia madoa kwenye matunda unatakiwa uwahi kupiga mapema maana bila hivyo habari ya MATUNDA 100 kwa mti utaisikia kwenye bomba. Changamoto nyingine ni kutopata mavuno tarajiwa ikiwa utazembea kumwagilia walau mara mbili au moja hata moja kwa mwezi ukikwama kabisa. Changamoto nyingine ni ikiwa utashindwa kuungana na masoko mapema maana yake matunda yanaweza kuozea shambani. Changamoto zingine zitategemea mahali unakolimia.
Umbali wa mche na mche nimetaja pale juu kuwa ni mita 2 kwa mbili ikiwa shamba hilo linaingia papai pekee pasipo kuchanganya na zao jingine lolote .
Duu! Kumbe imeshafika saa sita na mimi hapa upako haujakwisha, loooh! Hadi hapa naamini nimeshafanya kazi kubwa ya kwanza ya kukufanya uamini kwamba suala la kukamata milioni 890 ndani ya miaka mitano linawezekana na kupitiliza. Nilipanga kushusha data za strawberries kwa kina kama nilivyofanya papai, lakini muda umesonga na matirio ya papai yamefurika mno vichwani mwenu. Naona ni busara niwaache muendelee kuperuzi kwa kina kuhusu mapapai nami nitarejea wakati mwingine kwa strawberries. Ambapo ninataka kuzindua kampeni kwamba kila mbunge ni lazima alime strawberries maana hesabu zake zitakushangaza na kukuhamasisha pengine mara 10 ya hizi za mapapai. Pamoja na strawberries pia nitakuja na mikokotoo ya MATUNDA aina ya passion. Niwashukuru kwa kunifuatilia kwa umakini. Kama kuna mtu haamini kuwa inawezekana kupata milioni 890 ndani ya hii miaka mitano basi anione haraka nimkabidhi kwenye kamati ya maombi ya bunge wamuombee ajazwe Imani!
Wenu katika kuzisaka milioni 890
#Copy and paste

No comments:
Post a Comment