30.11.2018
UTUNZAJI
WA KUKU WANAOTAGA
MAHITAJI
YAO
Chakula
bora cha kuku wanaotaga (layer's mash) gram 120 kwa kuku kwa siku au nusu(1/2)
kwa kila kuku wanne kwa siku. Maji - wape maji safi na ya kutosha. Kinga dhidi
ya magonjwa kama vile kideri na gumboro kila baada ya miezi mitatu. Usafi wa
banda kwa
kuondoa
buibui, maranda yaliyolowa, kugeuza na kusawazisha maranda kila siku.
Usafi
wa vyombo vya maji na chakula. Hivi visafishwe kila siku.Kuzuia wadudu kama
viroboto na chawa au kuwaangamiza kila wanapoonekana.
Kuku
wasisongamane; kuku 3 - 4 katika kila meta moja ya mraba. Kuku wapewe majani ya
kula ili wasidonoane.
Wawekewe
viota vya kutosha, kwa wastani wa kiota kimoja cha
kutagia
kwa kila kuku watano. Kuku wawekewe bembea kwa ajili ya kupumzikia na kulala.
DALILI
AU MUONEKANO WA KUKU ASIYETAGA
1.
Kilemba kidogo, kinaonesha upungufu wa damu na kimesinyaa.
2.
Huonekana kama mgonjwa.
3.
Miguu yake humeremeta kwa mafuta.
4.
Nafasi kati ya nyonga ni ndogo. Nafasi kati ya kifua na nyonga ni ndogo.
Tumbo
dogo
na gumu.
5.
Njia ya kutagia (Kenti) ndogo, miringo na imesinyaa.
6.
Huita watoto na kuonesha hali ya kutaka kulalia mayai au kulea watoto.
UTUNZAJI
WA KUKU WANAOTAGA
MAHITAJI
YAO
Chakula
bora cha kuku wanaotaga (layer's mash) gram 120 kwa kuku kwa siku au nusu(1/2)
kwa kila kuku wanne kwa siku. Maji - wape maji safi na ya kutosha. Kinga dhidi
ya magonjwa kama vile kideri na gumboro kila baada ya miezi mitatu. Usafi wa
banda kwa
kuondoa
buibui, maranda yaliyolowa, kugeuza na kusawazisha maranda kila siku.
Usafi
wa vyombo vya maji na chakula. Hivi visafishwe kila siku.Kuzuia wadudu kama
viroboto na chawa au kuwaangamiza kila wanapoonekana.
Kuku
wasisongamane; kuku 3 - 4 katika kila meta moja ya mraba. Kuku wapewe majani ya
kula ili wasidonoane.
Wawekewe
viota vya kutosha, kwa wastani wa kiota kimoja cha
kutagia
kwa kila kuku watano. Kuku wawekewe bembea kwa ajili ya kupumzikia na kulala.
DK:
Mr Msuya
Mobile
no:0713573756
No comments:
Post a Comment