KILIMO BORA CHA SOYA :
Soya ni zao jamii ya mikunde ambayo ina baadhi ya sifa za mbegu zinazozalisha mafuta. Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya juu kuliko iliyoko katika aina nyingine ya mazao ya mimea. Kiasi cha protini katika soya inazidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa.
– Sentimeta 10 kwa #sentimita 60 kwa soya ndefu kama UyoleSoya1 na kwenye sehemu zenye rutuba nyingi.
– Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha sentimeta mbili hadi sentimita 5 ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama panya.
MBINU BORA ZA KUTUNZA SOYA BAADA YA KUVUNA
Soya ni zao jamii ya mikunde ambayo ina baadhi ya sifa za mbegu zinazozalisha mafuta. Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya juu kuliko iliyoko katika aina nyingine ya mazao ya mimea. Kiasi cha protini katika soya inazidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa.
Sifa nyingine za zao la soya ni pamoja na kuwa na mafuta yasiyo
kuwa na lehemu (cholesterol), uwezo wa mmea wa soya kuongeza mbolea aina
ya nitrojeni kwenye udongo, uwingi wa protini unaoweza kuondoa
utapiamlo hususani kwa watoto na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya
magonjwa.
Aidha, uwezo wa soya kustawi katika maeneo yanayostawisha mahindi
na maharage una maanisha kwamba zao hilo linaweza kulimwa sehemu nyingi
nchini Tanzania.
Sifa hizo zimefanya zao la soya kuwa muhimu katika chakula cha
binadamu na mifugo na katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za vyakula na
madawa. Vilevile gharama za uzalishaji wa soya ni ndogo ukilinganisha
na mazao mengine.
Pamoja na manufaa hayo ya zao la soya, zao hilo halifahamiki kama
ilivyo mazao mengine mfano maharage na mahindi. Wakulima wengi hawazijui
kanuni za kilimo bora cha soya. Hii inatokana na kutojua umuhimu wa zao
hilo na hivyo kutotilia maanani katika kulilima na kulitumia kuboresha
afya na kipato hasa katika ngazi ya kaya. Makala hii imeandaliwa maalumu
kwa ajili ya kumuelekeza mkulima jinsi ya kulima soya.
Soya ni zao linalostahimili ukame na huweza kulimwa kwenye maeneo
yenye mvua za kidogo, wastani hadi mvua nyingi kiasi vilevile soya
hufanya vizuri kwenye udongo wa tifutifu japo hufanya vizuri pia kwenye
udongo wa mfinyanzi.
Soya huhitaji wastani wa mililita 350 hadi 1,500 za
mvua kwa mwaka na inayonyesha kwa mtawanyiko mzuri hususani katika
kipindi chote cha ukuaji wa zao hilo. Soya pia inafaa katika kilimo cha
umwagiliaji kwani katika maeneo hayo kunakuwa na uhakika wa unyevu muda
wote. Jambo la kuzingatia ni kutowepo kwa mvua wakati soya inapokauka
3. KUANDAA SHAMBA
Shamba la soya linahitaji maandalizi mazuri kama ilivyo kwa mazao
mengine. Utayarishaji huo wa shamba ni pamoja na kuondoa magugu yote kwa
kuwa soya haivumilii magugu hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji
(seedling stage).
Shamba la soya linaweza kulimwa kwa sesa au matuta. Kilimo
cha sesa chaweza kulimwa kwa kutumia jembe la mkono au la kukokotwa
na wanyama kazi kama maksai na punda au kwa kutumia trekta. Kilimo cha
matuta kuzuia mmomonyoko wa udongo na kupunguza kasi ya maji kinafaa na
kinapendekezwa kwa maeneo yenye mwinuko
Vilevile kilimo cha matuta kinafaa sehemu tambarale lakini zenye
mvua nyingi ili kupunguza madhara ya maji yanayotuama baada ya mvua
kubwa kunyesha.
4. JINSI YA KUPANDA SOYA NA WAKATI SAHIHI WA UPANDAJI
Jambo la kuzingatia wakati wa kupanda ni kuhakikisha kuwa mbolea
haigusani na mbegu kwa sababu mbolea itaunguza mbegu na hazitaota.
Upandaji wa Soya hutegemea sana hali ya hewa ya eneo husika. Maeneo
yenye mvua nyingi Soya huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Novemba mpaka
katikati ya mwezi Desemba na Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa
mwezi February hadi March.
– Mkulima anashuriwa kupanda soya kwa nafasi zinazo pendekezwa na wataalamu. Nafasi hizo ni sentimeta 10 kwa sentimita 45 kwa soya fupi kama bossier na kwenye sehemu zenye rutuba hafifu.– Sentimeta 10 kwa #sentimita 60 kwa soya ndefu kama UyoleSoya1 na kwenye sehemu zenye rutuba nyingi.
– Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha sentimeta mbili hadi sentimita 5 ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama panya.
Mkulima ahakikishe kuwa soya inapandwa kwenye udongo wenye unyevu
wa kutosha; haitakiwi kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au
kuloweka soya kabla ya kupanda.
4.1 KIASI CHA MBEGU NA UPANDAJI WA SOYA
Ni muhimu kuandaa mbegu bora na safi mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa wastani kilo 20 hadi 30 za
mbegu za soya zinatosha kwa hekta moja kutegemeana na aina ya mbegu.
Kwa kuwa aina nyingi za soya hazistawi kila mahali, ni muhimu kwa
mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu inayofaa katika eneo analotaka
kulima soya hususani mahitaji ya mvua
4.2 MBOLEA
Kama ilivyo kwa mazao mengi, soya pia huhitaji udongo wenye rutuba
na usiotuamisha maji. Hivyo endapo soya italimwa katika sehemu yenye
rutuba hafifu, itahitaji mbolea kama mazao mengine ijapokuwa huvumilia
udongo wenye rutuba hafifu.
Kwa hiyo uamuzi wa kutumia au kutotumia mbolea na kiwango cha
kutumia utategemea rutuba iliyopo kwenye udongo katika eneo husika.
Hata hivyo, soya huhitaji wastani wa kilo 80 hadi 100 za mbolea aina ya DAP na TSP kwa hekta moja na kilo 60 hadi 80 kwa mbolea aina ya CAN kwa hekta moja (Heka 2 na Nusu).
4.3 KUZUIA MAGUGU
Soya ni zao ambalo huzongwa na magugu hususani ikiwa katika hatua
za mwanzo za ukuaji. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi palizi katika
kipindi cha wiki mbili baada ya soya kuota. Palizi ya mara ya pili
inategemeana na kiwango cha magugu shambani. Endapo magugu yatakuwa
yamefunikwa na majani ya soya palizi ya pili inaweza isihitajike.
Magugu katika shamba la soya yanaweza kudhibitiwa pia kwa katumia dawa ya kuzuia magugu kama GALEX; hata hivyo inafaa kufuata maelekezo ya kutumia ya dawa husika yaliyopo kwenye kibandiko
5. MAGONJWA, WADUDU NA VIUMBE WANAOSHAMBULIA SOYA
- MAGONJWA
Tofauti na mazao mengine, magonjwa ya soya ni machache. Hata hivyo
magonjwa ambayo hutokea kwa nadra ni yale yanayotokana na vimelea vya
ukungu na bakteria. Magonjwa hayo huenezwa kwa mbegu, masalia ya mimea
shambani na wadudu mafuta.
Njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo katika zao la soya
ni kupanda mbegu safi na zilizopendekezwa mahali husika. Aidha, panda
kwa mzunguko (crop rotation) kwa kutumia mazao yasiyoshambuliwa na
magonjwa ya soya kama alizeti na mahindi.
- WADUDU WAHARIBIFU KWENYE SOYA
Soya haishambuliwi sana na wadudu kama ilivyo sehemu nyingine
ambako zao hilo hulimwa kwa wingi. Hata hivyo endapo wadudu watatokea
mkulima anashauriwa kutumia dawa za wadudu kama Thiodan 35% EC na Sumithion 50% EC kwenye kipimo cha mililita 40 za dawa na lita 20 za maji au kipimo kinacho pendekezwa katika dawa husika.
Upuliziaji wa dawa ufanywe kulingana na kiasi cha mashambulizi ya wadudu kwenye mazao.
Hakuna wadudu waharibifu wa soya ghalani. Hivyo zao hilo linaweza
kutunzwa kwa muda mrefu ghalani bila kuwa na athari za wadudu. Kwa
mkulima na wafanyabiashara, kutokuwepo wadudu waharibifu ghalani
kunapunguza gharama za utunzaji hadi bei nzuri itakapofikiwa. Wanyama
waharibifu
5.3 WANYAMA WAHARIBIFU KWENYE SOYA
Kwa kawaida soya hupendwa sana na panya wa shambani na ghalani.
Wanyama wengine ni pamoja na sungura, paa, swala, Ngedere n.k. Mkulima
anashauriwa kutumia mbinu na njia mbalimbali zikiwemo za asili,
kukabiliana na wanyama hao bila kuharibu mazingira.
UVUNAJI WA SOYA
DALILI ZA KUKOMAA
Dalili za soya kukomaa ni wakati majani yanapokuwa na rangi ya
njano. Mkulima anashauriwa kuanza kuvuna baada ya majani kuanza
kupukutika.
Baada ya soya kupukutisha majani shambani mkulima anatakiwa kung’oa
soya kwa kutumia mikono au anaweza kuvuna kwa kutumia mashine maalumu
za kuvunia.
7.1 KUPURA
Soya haitakiwi kupigwa kwa nguvu kwa sababu mbegu zake hupasuka
kirahisi. Mara baada ya kupura, ondoa takataka na uchafu mwingine kwenye
soya kwa kupepeta na kupembua. Kisha Kausha soya kufikia wastani wa
asilimia 10 ya kiasi cha maji/unyevu (moisture content) kisha ihifadhi
ghalani kwa matumizi au kusubiri soko.
7.2 KUHIFADHI
Soya ikikauka, maganda yake hupasuka na mbegu hupukutikia chini.
Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi kuvuna soya mara inapokomaa na
kuanza kukauka. Ili kuzuia upotevu wa zao shambani, inashauriwa kuvuna
majira ya asubuhi au majira ambayo sio ya jua kali endapo soya imekauka
na kuanza kupasuka wakati wa kuvuna.
Wataalamu wa uhifadhi bora wa mazao wanashauri kuwa ni vyema mazao
yakawekwa juu ya mbao au vichanja maalumu vijulikanavyo kama pallets.
Hivi vinazuia soya kuharibika na kukosa bei nzuri sokoni. Vile vile
ghala linapaswa kuwa na sifa bora kama kutokupitisha wadudu waharibifu,
paa lisilovuja na mzunguko mzuri wa hewa ili kufanya soya iliyohifadhiwa
ikae kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment