Mazao ya Kilimo Yalivyo na Tija katika swala la urembo . - Dar East Project

Post Top Ad

Mazao ya Kilimo Yalivyo na Tija katika swala la  urembo .

Mazao ya Kilimo Yalivyo na Tija katika swala la urembo .

Share This
Watu wengi tumekuwa hatujui kuwa vitu tunavyokula vinaweza kuleta athari kubwa karibia katika kila sehemu ya mwili wetu,na sio desturi kwa wengi wetu kula matunda kwa wingi, lakini matunda ukiachana na kuongeza virutubisho katika mwili  pia yanasaidia kuweka ngozi ya mwanadamu kuwa laini.
Avocado
Ni moja ya tunda maarufu sana ktika utengenezaji wajuice, lakini wengi wao hawawezi kula hivihivi kutokana na kutokuwa na radha halisi.unashauriwa kula na kunywa jice ya tunda hili mar nyingi uwezavyo ili kusawazisha mafuta mwili.lakini pia usaidia kuongeza uzito mwilini.
Apple
wengi ulihusisha sana na mambo ya mapenzi,ni moja ya tunda lenye bei kali na lenye umaarufu mkubwa ulimwenguni.apple ufanya kuwepo na mzunguko mzuri wa damu mwilini na kuhifadhi ngozi uhalisia wa ngozi.
Ndizi
Ni tunda linalopendwa na watu wengi ulimwenguni kwa sababu ya radha yake ya sukari,ukiachana na kuasaidia katika mmengenyo wa chakula lakini pia ndizi usaidia sana kuboresha ngozi iliyokauka, ndio maana baadhi ya losheni utengenezwa na tunda hili.
Papai
papai husaidia kukupa ngozi ya mafuta,kuziba na kurudisha sehemu zilizoumia au kunyofoka.Pia ungarisha ngozi kutokana na enzymes inayotoka katika papai inayoitwa Papain, kwa wale wenye shida ya ngozi ya usoni wanashauriwa kupaka papai lililochanganywa na asali katika uso.
Chungwa

Chungwa husaidia kurudisha ngozi iliyoharibika na kuipa ngozi uhalisia wake.Ukitaka kutumia chungwa usoni, chukua juisi ya chungwa Paka usoni kaa nayo dakika kumi alafu osha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here