Fifa Wateuwa Waamuzi 18 Kutoka Tanzania - Dar East Project

Post Top Ad

Fifa Wateuwa Waamuzi 18 Kutoka Tanzania

Fifa Wateuwa Waamuzi 18 Kutoka Tanzania

Share This


Jumla ya waamuzi 18 wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kuchezesha mechi za kimataifa kwa mwaka 2019.


Katika orodha hiyo wapo waamuzi wa katikati na Waamuzi wasaidizi wa Kiume na wa Kike pamoja na waamuzi watakaochezesha mechi za soka la Ufukweni.

Waamuzi wenye beji za FIFA ni waamuzi wakuu, yaani waamuzi wa kati ni wanne tu upande wa wanaume, wakati sita ni waamuzi wasaidizi, maarufu kama washika vibendera.

Waamuzi wa katikati Wanaume ni Mfaume Ali Nassoro, Hery Ally Sasii, Emmanuel Alphonce Mwandembwa na Martin Elifhas Saanya, wakati Waamuzi Wasaidizi ni Ferdinand Chacha, Mgaza Ally Kinduli, Soud Iddi Lila, Frank John Komba, Mohamed Salim Mkono na Mbaraka Haule.

Waamuzi wa kike wa Katikati ni Jonesia Rukyaa Kabakama na Florentina Zabron Chief, wakati waamuzi wasaidizi wa kike ni Hellen Mduma Joseph, Grace Wamala, Janet Charles Balama na Mtwana Dalila Jafari na Waamuzi wa soka la Ufukweni ni Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here