Zijue Aina za Kuku na Faida Zake Katika Ufugaji - Dar East Project

Post Top Ad

Zijue Aina za Kuku na Faida Zake Katika Ufugaji

Zijue Aina za Kuku na Faida Zake Katika Ufugaji

Share This
                                                          
                                                          

Kuna aina mbalimbali za kuku ambazo mfugaji anaweza kufuga na kila aina inategemeana na malengo ya mtu husika anayetaka kufanya shughuli hii ya ufugaji,Lakini hapa tunaangalia  makundi makuu manne ya kuku ambayo tunayafuga  sawa kwa Tanzania.

  • KUKU WA NYAMA.
Hii ni moja ya kundi la kuku ambalo linafugwa sana hapa nchini na kuku hawa wanafugwa kwa malengo ya kuzalisha nyama tu. Uzalishaji wa kuku hawa wanachukuliwa kuku wazazi kutoka nje ya nchi na kuhifadhiwa sehemu maalumu kwa ajiri ya kuzalisha mayai na mayai yanatotoreshwa na kupata vifaranga kwa ajili ya nyama ,

Faida ya kuku hawa.
 kuku hawa hufugwa kwa mda mchache muda wa miezi miwili au mitatu na kuuzwa kwa ajili ya matumizi ya nyama, hivyo ni sehemu nzuri ya kujipatia pesa kwa muda mfupi.

Hata hivyo, Gharama za kuwalea kuku hawa ni kubwa kidogo hivyo unapoamua kufanya ufugaji kwa ajili ya kupata tija katika kukuza kipato chako ni muhimu ukafuga kuku wengi kwa wakati mmoja hii itakufanya upate faida nzuri kuliko kufuga kuku wachache .

  • KUKU WA MAYAI.
Ni aina ya kuku ambao hufugwa kwa malengo maalumu ili kuzalisha mayai, kuku hawa wanataga kwa wingi sana mayai na wanataga bila jogoo, kuku hawa wamendaliwa vizuri kwa ajili ya kutaga tu hivyo kama utaamua kuwawekea jogoo watataga na kuatamia  lakini vifaranga wake watakuwa hawana ubora ule unaotakiwa.

Faida .

Kwakuwa kuku hawa ni watagaji wazuri wa mayai basi wanampatia mfugaji uhakika wa kipato kwa kila siku hadi pale atakapofikia mwisho wa mradi wake, ambapo mara nyingi huwa ni  miaka miwili.

Zingatia.
Ili kupata faida iliyokusudiwa katika mradi wako huu wa kuku unatakiwa uwape chakula bora na cha kutosha pia  uzingatie chanjo na tiba kwa magonjwa pale unapoona dalili ya magonjwa.

  • KUKU CHOTARA.
Hawa ni aina ya kuku ambao wamechanganya aina fulani ya kuku na aina nyingine ya kuku na kupata aina moja ya kuku, mfano: amechukuliwa jogoo  wa kienyeji akachanganywa na tetea wa kisasa na  vifaranga vitakavyotoka vitakuwa chotara kwa maana watakuwa na sifa baadhi za kienyeji na sifa baadhi za kisasa.

Kuku hawa kwa hapa nchini wapo wengi na kuna makundi mbalimbali ya kuku kulingana na asili na mahali walipo tokea, mfano: MALAWI, KENBRO, SASO na KROILA na hawa wanatofautiana sifa na asili.

Faida ya kuku chotara.

  1. Wanakuwa kwa haraka na wanakuwa na maumbo makubwa tofauti na kuku wakienyeji hivyo ni wazuri sana kwa nyama.
  2. Ni watagaji wazuri sana tofauti na kuku wakienyeji (kuku hawa ukuwahudumia vizuri wanataga mayai kati ya 180-300 kwa mwaka hivyo ni wazuri sana kwa mayai.
  3. Wanaishi kwenye mazingira yeyote yale kwa maana wanaweza kuishi vizuri wakiachiwa kujitafutia chakula.
  4. Wanastahimili sana magonjwa (chanjo ni Muhimu kuwapa)  tofauti na kuku wa nyama au wa mayai.
  5. Nyama yao ni nzuri sana haina tofauti na kuku wakienyeji.
  6. Wanauzito  mkubwa kuku mmoja anafika hadi kilo sita.
  7. Soko lake ni kubwa.
  • KUKU WA KIENYEJI.
Hawa ni kuku ambao asili yake ni hapa hapa Tanzania na tunao katika maeneo mengi ya nchi yetu, kuku hawa wanakuwa wana maumbo madogo kulinganisha na kuku chotara, pia kuku hawa  hawakui kwa haraka ukilinganisha na kuku chotara,  aina hii ya kuku hutaga mayai machache sana kwa mwaka na wanataga mayai kati ya 40-120.

Faida .
Kuku hawa wanafugika katika mazingira yeyote yale kwa sababu ni wazuri kujitafutia chakula, ili upate faida nzuri ya mradi wako wa kuku huo unashauriwa kuwapa chakula cha ziada ili waweze kukua kwa haraka na kuwa na uzito mzuri.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here